NGISI YA KUSALI RSARIO  1. Alama ya Msalaba 2. Sala ya kutubu 3. Somo la tendo la kwanza la siku 4. Baba Yetu Na Kwamwakia Maria (10x) Sifa kwa Baba 5. Kuisali kwa kila tendoA répéter pour chacun des cinq mystères du jour 6. Sala kwa Bikira Maria ALAMA YA MSALABAKwa alama ya Msalaba Mtakatifu, utuokowe Bwana na maadui zetu. Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amen. SALA YA KUTUBUMungu wangu, ninauzunika sana zambi zangu nyingi sana na ukosefu wa ukamilifu. Ninakuomba huruma kwa zambi zangu zote za maisha yangu, hasa zile za siku ya leo. Ninanungunika zambi zangu kwa sababu nimekukosea, Wewe Mungu wangu, nimpende yesu kuliko vitu vyote, na kwa sababu zambi zinaumiza Moyo wake Mtakatifu, Moyo wako Mtakatifu, O Yesu. Unihurumie, Moyo Mnyenyekevu wa yesu ; unitakase kwa zambi zangu zote na uniimarishe kwa neema yako na nikuusudie kutenda tena zambi, nikiungama na nikiepuka vishawishi vyote vya zambi. Amen SIFASifa kwa Baba na kwa Mwana na kwa Roho Mtakatifu Kama ilivyo kuwa mwanzo na sasa na siku zote na miaka ya milele. Amen. BABA YETU Baba yetu uliye Mbiguni, jina lako lisifiwe, Ufalme wako uje, duniani kama mbinguni Utipe leo chakula chetu cha kila siku. Utusamee makosa yetu, kama tunavyo wasamee waliyo tukosea, usitwache kushinda na vishawishi, lakini utuopowe katika maovu. Amen SALAMU MARIANakwamkia Maria, umejaliwa neema, Bwana yu nawe, mbarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na mbarikiwa mtoto wa tumbo lako, Yesu. Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na wakati wa kufa kwetu. Amen. MAFUMBO YA UTUKUFU1.Yesu anafufuka. Yesu, siku ya tatu baada ya kufa kwako, ulifufuka katika wafu. Nao Mitume waliokuona baada ya ufufuko wako walijitolea maisha yao kwa kulinda imani hii. Naamini, pia, kwamba kifo sio mwisho wa maisha. Nipe neema niwe na roho safi na nyofu, kama yako, ili nifuate njia yako inifikishayo kwa ufufuko na furaha ya milele. 2.Yesu anapaa mbinguni. Siku arubaini baada ya ufufuko wako, ulipaa mbinguni. Pia sisi twatamani kuende mbinguni. Tunataka kuishi kulingana na maadili yako. Lakini hatuwezi hayo bila usaidizi wako. Tafadhali tupe nguvu ya kustahilisha vipaji Mungu alivyopanda nyoyoni zetu vienee kila siku. 3.Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Maria, wakati uliomba na Mitume Roho Mtakatifu aliwabadili, wakajawa na ushujaa, na wakaenda kulieneza neno la Yesu lijulikane duniani kote. Tunaposali rosari, tafadhali omba nasi ili Roho Mtakatifu afungue milango ya roho zetu. Funza watoto wa dunia ya kisasa kusali rosari na kuishi kwa kukubaliana, ili Roho Mtakatifu awafanye watume wa upendo wa Mungu na wenye furaha. 4.Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Maria, Mungu alikuchukua kwa Moyo na Mwili akakupaliza mbinguni na akakupatia kazi ya kutuleta kwa Yesu, kutuongoza, na kutulinda. Mama, nakupatia roho yangu. Nataka kuishi pamoja nawe, na kushirikiana nawe. Nataka roho yako iwe kimbilio na njia yakunipeleka kwa Mungu. 5.Bikira Maria anavikwa Taji kuwa Malkia wa Mbingu na Inchi. Mama, tunataka kufuata njia yako kama tuifuatayo kwa rosari. Tunataka kuendelea mbele na maisha tukiwa na nguvu, ustahili, ukarimu, unyenyekevu, na kushirikiana kwa upendo, amani na furaha. Tunakuvisha Taji uwe Malkia wa roho zetu, na tunakuomba utuongoze na utubadili. Tunakuomba utusaidie kutafuta Mwanao ili tuwe na furaha. Matendo ya furaha (Siku ya Kwanza na ya Posho) 1. Maria amepashwa na Malaika kama  atakuwa Mama wa Mwokozi. 2. Maria anamtembelea Elisabeth. 3. Kuzaliwa kwa Bwana Yesu Betlehemu. 4. Kutolewa kwa Bwana Yesu Ekaluni. 5. Maria amemktuta Yesu Ekaluni. Matendo ya Mwanza (Siku ya Ine) 1. Yesu amebatizwa katika mto wa Yordani. 2. Sheree ya ndoa Kana. 3. Kutangazwa kwa Ufalme wa Mungu. 4. Yesu amegyeuka uso. 5. Kusimikwa kwa ukaristia. Matendo ya uchungu (Siku ya Pili na ya Tano) 1. Yesu anasali katika bustani ya Gethsémani. 2. Yesu anapigwa na waaskari. 3. Yesu anavikwa taji la miiba kichwani. 4. Yesu anachugua Msalaba wake. 5. Yesu anasulubia msalani. Matendo ya Utukufu (Siku ya Tatu na ya Mungu) 1. Yesu amefufuka. 2. Yesu amepanda Mbinguni. 3. Yesu amewapelekea Mitume Roho Mtakatifu. 4. Mama Maria amepalizwa Mbinguni. 5. Mama Maria amevikwa Taji la Umalkia wa Mbingu na Dunia.
|