|
JINZI YA KUSALI ROSARI  1. Ishara ya Msalaba 2. Kanuni ya Imani 3 Atukuzwe Baba 4. Kutangaza Fumbo(Tendo) 5. Baba Yetu Salamu Maria (10x) Atukuzwe Baba 6. Salamu Malkia ISHARA YA MSALABA Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina KANUNI YA IMANI Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenye zi, Muumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu ; aliyetugwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa ; akashukia kuzimu siku ya tatu kafufuka katika wafu ; akapaa mbinguni ; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi ; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu . Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki,ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele. Amina. . Amén. ATUKUZWE BABA Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele. Amina. BABA YETU Baba yetu uliye Mbiguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliyotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopowe maovuni. Amina. SALAMU MARIA Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa wa kufa kwetu. Amina. MAFUMBO YA FURAHA 1. Malaika anampasha habari Maria kwamba atakuwa mama wa Mungu. "Salamu Maria! Bwana yu nawe!" Kupitiya maneno haya, Malaika amekusalamu Maria, na amekupasha kama Bwana amekuchagua kuwa Mama wa Mkombozi. Vile vile Bwana amekuchagua nasi kati ya watoto wake ili tuwe Mitume wa Amani duniani hii. 2. Maria anakwenda kumtembelea Elisabeti. Maria: Kisha kupokea maagizo ya Malaika, umeenda kumtembela ndugu yako Elisabeti kwa kumsaidia kazi. Umechukua tumboni mwako Yesu, umeleta uwokovu, na juu ya hiyo, nyumba ya Elisabeti imejazwa furaha na amani na imebadirika. Tunatamani nasi dunia, nchi yetu, jamaa letu na maisha yetu yabadirishwe na yajazwe na furaha 3. Yesu anazaliwa Betlehemu
Bwana Yesu, umekuja duniani katika unyenyekevu wa zizi la Betlehemu, ili utuokoe na ubaki daima nasi– Tunakushukuru. Maria, wewe uliyetayarisha zizi la Betlehemu, utayarishe pia nyoyo chetu ili tuwapende marafiki, ndugu zetu na tusiite hata mtu mmoja adui. 4.Yesu anatolewa hekaluni. Maria: Umemleta mwana wako Hekaluni ili umtolee kwa Mungu. Sisi pia tuo watoto wako. Umtolee Mungu Baba yetu, hatua hii ya sala ya « Umoja wa Watoto Milioni Moja kwa kusali Rosari » ili atujaliye Umoja na Amani ndani ya jamaa zetu, katika Nchi yetu na katika Dunia nzima. 5. Maria na Yusufu wanamkuta Yesu hekaluni Maria: Wakati hakumuona Yesu tena, alimtafuta bila kuchoka muda wa siku tatu.. Mama: Watu wengi wanamsahau Yesu na wanakosa Amani, Furaha na Mapendo yake. Tunakuomba uwasaidie ili wampate Yesu tena na waishi heri yao. Matendo ya furaha (Siku ya Kwanza na ya Posho) 1. Maria amepashwa na Malaika kama atakuwa Mama wa Mwokozi.  2. Maria anamtembelea Elisabeth. 3. Kuzaliwa kwa Bwana Yesu Betlehemu. 4. Kutolewa kwa Bwana Yesu Ekaluni. 5. Maria amemktuta Yesu Ekaluni. Matendo ya Mwanza (Siku ya Ine) 1. Yesu amebatizwa katika mto wa Yordani. 2. Sheree ya ndoa Kana. 3. Kutangazwa kwa Ufalme wa Mungu. 4. Yesu amegyeuka uso. 5. Kusimikwa kwa ukaristia. Matendo ya uchungu (Siku ya Pili na ya Tano) 1. Yesu anasali katika bustani ya Gethsémani. 2. Yesu anapigwa na waaskari. 3. Yesu anavikwa taji la miiba kichwani. 4. Yesu anachugua Msalaba wake. 5. Yesu anasulubia msalani. Matendo ya Utukufu (Siku ya Tatu na ya Mungu) 1. Yesu amefufuka. 2. Yesu amepanda Mbinguni. 3. Yesu amewapelekea Mitume Roho Mtakatifu. 4. Mama Maria amepalizwa Mbinguni. 5. Mama Maria amevikwa Taji la Umalkia wa Mbingu na Dunia.
|